Kwa kipindi kirefu Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe hajawa kwenye uhusiano mzuri na nchi za Ulaya na Marekani… upande wa pili Rais huyo amekuwa rafiki mkubwa sana na nchi ya China, na ndiko misaada mingi inakotokea kuingia Zimbabwe.
Vichwa vya habari za kimataifa kwenye mitandao mikubwa vimeandika kwamba huenda Zimbabwe wakahalalisha pesa ya China ianze kutumika Zimbabwe kama vile ambavyo pesa yao ya ‘Zimbabwean Dollar‘ inatumika kwenye mzunguko wa kila siku !!
Tuliwahi kusikia mara kadhaa Wabunge wa TZ wakilalamika na kuitaka Serikali kuzuia matumizi ya dola kwenye manunuzi ya bidhaa ndani ya nchi, lakini kwa Zimbabwe mipango ndio iko hivyo.
Zimbabwe imesamehewa deni la dola milioni 40 (hiyo ni zaidi ya Bilioni 80 za Kitanzania) kutokana na msamaha huo, Waziri mmoja Patrick Chinamasa amesema huenda wakapitisha utaratibu wa pesa ya China ambayo ni Yuan ikaingia kwenye mzunguko wa pesa za nchi hiyo na kutumika kwenye matumizi ya kawaida kama njia ya kuboresha uhusiano mzuri wa kibiashara kati ya Zimbabwe na China.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE