Nchi ya Zimbabwe imeingia katika mfungo wa maombi ya siku tatu kuanzia ili kujinusuru na janga la Corona linalowatafuna.
Maombi hayo ya siku tatu yanaongozwa na mke wa Rais wa nchi hiyo Auxillia Mnangagwa na yatamalizika kesho kutwa Jumamosi kwa maombi ya kushukuru ili kuepukana na janga hilo.
Mke huyo wa Rais Emmerson Mnangagwa amewaomba wanawake wote wa Zimbabwe na walio nje ya Zimbabwe kuungana nae katika maombi hayo akisema “Tunahitaji kufanya mkakati madhubuti kuanzia nyumbani, kunawa mikono, kuvaa barakoa sahihi cha msingi zaidi kila mmoja azingatie kanuni za afya na kuwa salama kwa kuepuka misongamano.”
Takwimu za nchi hiyo zinaonyesha kuwa jumla ya watu waliombukizwa virusi vya Corona ni 29,408, watu 879 wakifariki na watu 19,253 wakipona.