Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa umoja wa kamati za mahesabu za nchi za Afrika(Afropac) ambapo muda mfupi baadae aliandika kuhusu hicho cheo kipya kwenye page yake facebook.
>>> Umoja wa Kamati za Mahesabu ya Serikali ya nchi za SADC (SADCOPAC) umenichagua kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Kamati za Mahesabu za Nchi za Afrika (AFROPAC) kuziba nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Msumbiji.
Ni dhahiri mapambano dhidi ya ufisadi katika bara la Afrika yatafanikiwa iwapo mabunge ya wananchi yanasimamia vema serikali. Ni heshima kubwa kwa nchi yangu kupata fursa hii ya kujenga utamaduni wa uwajibikaji kupitia kamati za BUNGE za mahesabu. Ni changamoto kubwa ninayoipokea kwa unyenyekevu mkubwa. Kuwa Katibu Mkuu wa AFROPAC ni fursa ya kujitoa kujenga Afrika Mpya yenye kujali rasilimali za umma kama Mali ya wananchi. Mungu atanilinda na kunisaidia katika kutimiza wajibu huu.
Unataka kuwa karibua na kila stori inayonifikia? jiunge nami twitter kwa kubonyeza HAPA, facebook na Instagram bonyeza HAPA na HAPA kujiunga na mimi pia.