Wakati wabunge wakiendelea kuchangia hoja kuhusu bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameomba Bunge kutoipitisha bajeti hiyo na kusema…
>>>’Adhma ya nchi yetu kuwa ya Viwanda ni adhma yetu sote. Jambo hili ni jambo la Maendeleo na halina ushabiki wa kivyama. Tumepitisha Mpango wa Maendeleo katika Bunge hili na kwa hiyo ni Mpango wa Nchi sio mpango wa vyama tena‘
‘Sekta ya Viwanda na Sekta ya Kilimo kwa pamoja zinachangia nusu ya Pato la Taifa ( GDP) na nusu nyingine ni sekta ya Huduma. Nadharia za Uchumi zinatuambia kuwa Tija ikiongezeka kwenye ya Kilimo inawezesha sekta ya Viwanda kukua na kisha sekta ya Huduma‘
‘Sekta za kuondoa umasikini ni Kilimo na Viwanda hivyo lazima mikakati ya Serikali iendane na kufungamanisha haya. Ndio Maana Nchi nyengine Wizara ya Kilimo hujumuisha uongezaji thamani ( Ministry of Agriculture and Agro-processing ). Hatuhitaji kufanya hivyo, tunachohitaji ni kufungamanisha‘
‘Hata hivyo Serikali imeshindwa kufanya hivyo katika mwaka wake wa kwanza tu wa Bajeti. Nitaeleza kwa kutumia changamoto tuliyonayo kuhusu Sukari, Mafuta ya Kula na Nguo.’
‘Ukitazama hotuba ya Waziri wa Kilimo ambayo Bunge lako tukufu limeshapitisha bajeti yake kuna ‘mikakati’ ya kulima Miwa kwa ajili ya Sukari. Ukurasa wa 44 ibara ya 107 ya Hotuba ya Wizara ya Kilimo na ukurasa wa 25 ibara za 63 na 64 zinaeleza ‘mikakati’ ya kukabiliana na uhaba wa Sukari nchini.’
‘Mheshimiwa Spika, nashauri Bunge lako tukufu leo lisipitishe Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili Wizara hii ikakae na Wizara ya Kilimo wawianishe mipango hii na kisha walete hapa Bungeni ndio tupitishe.‘
ILIKUPITA KATIKA MASWALI NA MAJIBU BUNGENI LEO, WAZIRI MWIJAGE KAYAJIBU HAYA?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE