Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Man United wamekubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Hull City

on

Usiku wa January 26 2017 kocha Jose Mourinho alikiongoza kikosi chake cha Man United kuingia katika uwanja wa Kingston Communications unaotumiwa na Hull City kucheza mchezo wao wa EFL Cup.

Man United wakiwa ugenini licha ya kuwa na kikosi chao kikiwa na staa ghali zaidi duniani Paul Pogba, walijikuta wakipata kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Hull City, licha ya Paul Pogba kuisawazishia goli Man United dakika ya 66, baada ya Tom Huddlestone kuifungia Hull City goli la uongozi dakika ya 36.

Dakika ya 85 ilikuwa mbaya kwa Man United baada ya El-Hadji Baye Niasse kuifungia goli la ushindi Hull City, licha ya Man United kuwa na wachezaji wao nyota kama Paul Pogba na Rashford hawajafanikiwa kuinusuru Man United na kipigo licha ya kuwa wamefuzu kucheza fainali dhidi ya Southampton waliyowatoa Liverpool.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement