PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Baada ya kubeba tuzo, Monalisa amefunguka kuhusu ‘shavu’ la Ubalozi

on

Msanii wa filamu nchini, Yvone Cherrie ‘Monalisa’ amezungumzia suala la kuwa balozi wa Sadaka Network ikiwa na lengo la kuwasaidia wanawake na watoto waliopatwa na matatizo yanayohitaji huduma za Kiafya.

Monalisa ambaye miezi michache iliyopita alibeba tuzo ya Msanii bora wa Kike Afrika, amesema amechaguliwa kuwa balozi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wanaonyanyaswa kijinsia na wenza wao pamoja na watoto wanaokumbwa na majanga ikiwemo kumwagikiwa na maji ya moto.

Monalisa amesema kutokana na hatua hiyo kuna jopo la madaktari bingwa kutoka nje ya nchi ambapo watakuja nchini kwa ajili ya kuwafanyia matibabu wanawake na watoto waliokumbwa na matatizo -ya namna hiyo kutoka mikoa mbalimbali.

“Nikiwa kama balozi nipo hapa kwa ajili ya kuhamasisha jamii, kuwaomba kuchangia kile kidogo walichonacgo ili kurudiha tabasamu kwa wamama na watoto kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania,”amesema.

EXCLUSIVE: MONALISA AFUNGUKA KUWA MWALIMU, AWASHANGAA WANAOPENDA ‘KIKI’

BREAKING: MBOWE apelekwa Dubai kimatibabu, wenzake wasomewa maelezo ya awali

Soma na hizi

Tupia Comments