Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Utashangazwa na bei ya Biblia iliyokutwa nyumbani kwa Whitney Houston

on

Ifahamu thamani ya biblia iliyokutwa ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi marehemu Whitney Houston ambayo inasemekana kuuzwa dola za Kimarekani elfu 95 ambazo ni zaidi ya shilingi Milioni 200 za Kitanzania.

Marehemu Whitney Houston alihamia katika nyumba hiyo mwaka 2009 na baada ya mwaka mmoja alifariki dunia, mwenye nyumba hiyo aliyokuwa akiishi marehemu amedai kuwa alikuta biblia katika box ambalo lilikuwa na baadhi ya vitu alivyoviacha Whitney wakati anahama na alimshirikisha Manager wa Marehemu kuhusiana na vitu hivyo lakini aliambiwa abaki navyo kama anavitaka.

Baada ya maamuzi yaliyotolewa na Manager, mwenye nyumba huyo aliamua kuongea na kampuni ya ‘Moments in Time’ inayohusika na kupiga mnada na kufikia kuuza biblia hiyo kwa gharama ya dola elfu 95 za Kimarekani ikiwa vitu vingine aliamua kuviweka pembeni.

Nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Whitney Houston

Marehemu Whitney Houston alifariki dunia February 11,2012 akiwa na umri wa miaka 48 baada ya sababu ya kifo chake kutajwa kuwa ni ugonjwa wa moyo na matumizi ya dawa za kulevya aina ya ‘Cocaine’

Ulivyopokelewa mwili wa ‘Sam wa Ukweli’, Mastaa waliohudhuria

 

Soma na hizi

Tupia Comments