Premier Bet

Habari za Mastaa

BASATA imefungia wimbo wa Mbunge Sugu

on

Moja ya taarifa ambayo imetolewa na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) leo June 19, 2018 ni pamoja na hii ya kuufungia wimbo wa Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu wa #219 na sababu ya kuufungia ikitajwa kuwa ni uchochezi na kuhatarisha amani.

Pamoja na kuufungia wimbo huo BASATA inamuonya Sugu na kumwagiza kuacha mara moja kujihusisha na kutangaza au kusambaza wimbo huo, kwani baraza hilo limekuwa likipokea simu za maswali na malalamiko kutoka kwa wadau wa sanaa walionoesha kuchukizwa na kuguswa na wimbo huo.

Hata hivyo BASATA imesema haitawavumilia wasanii wachache wanaotaka kugeuza sekta ya sanaa kama kichaka cha kusambaza sumu kwa lengo la kuigawa jamii na kuharibu amani.

Benson aliyeimba ‘HAUZIMI’ kutoka uhudumu wa Bar mpaka malengo haya

Soma na hizi

Tupia Comments