Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Sugu avutiwa na upambanaji wa Jay Z, amuita mwanae ‘Shawn’

on

Siku kadhaa zilizopita Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu alibahatika kupata mtoto wa kiume pamoja na mpenzi wake Happiness na hivyo ameamua kumpa mtoto wake huyo jina la Shawn ikiwa na maana kuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Sugu ameweka wazi sababu nyingine ya kumuita mtoto wake Shawn ambapo amesema ni katika kumuenzi rappa wa Marekani Jay Z ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter akiwa amevutiwa na upambanaji wake katika maisha hadi kufikia hapo alipo na kutambulika na dunia nzima kwa ujumla.

“Tumempa mtoto wetu jina SHAWN JOSEPH MBILINYI…SHAWN (Tamka SHON) lina maana ZAWADI TOKA KWA MUNGU ( A GIFT FROM GOD)…Pia ni katika kumuenzi Msanii na Mfanyabiashara maarufu duniani JAY-Z, ambaye jina lake halisi ni SHAWN CARTER… Hii ni kutokana na jinsi FALSAFA zake kuhusu HUSTLING zilivyonisaidia kufika hapa nilipo kwenye maisha. Asanteni sana… #JONGWE #MVMP #MisutiKabatini” >>>aliandika Sugu 

AUDIO: SHAMSA FORD AJITANGAZA KUWA SINGLE “MA-SINGLE LADIES TUAKATAFUTE HELA”

Soma na hizi

Tupia Comments