Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Tyga ampa heshima hii kubwa Lil Wayne kwenye ‘Lightskin Lil Wayne’ (+Video)

on

Siku ya Jumatatu July 8,2019 Rapper Tyga aliachia ngoma yake ya ‘Lightskin Lil Wayne’ ambapo ndani ya ngoma hiyo amempa heshima kubwa mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Lil Wayne.

Ukiiangalia vizuri ngoma hiyo Tyga amechanganya mawazo ya Lil Wayne kwenye video 3 ambazo Lil Wayne alizifanya enzi zake ikiwemo ngoma ya A Milli, Fire Man na Lollipop. Lil Wayne pia amekubali kile ambacho Tyga amekifanya na kuenzi nyimbo zake kwa ujumla.

“Upendo!!!, hii ni nzuri sana kaka, nimeishiwa maneno baada ya kutazama na kusikiliza hii nyimbo, najiskia kuwa na faraja kubwa baada ya kuheshimiwa kwa njia hii na ni vizuri zaidi ikiwa imetoka kwako” >>>aliandika Lil Wayne kupitia ukurasa wake wa instagram.

AUDIO: MREMBO TUNDA NA WHOZU MAMBO HADHARANI “NIMECHAGUA LOVE SIO PESA”

Soma na hizi

Tupia Comments