Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Vera Sidika kajibadilisha rangi, Eric Omondi ameshindwa kuvumilia (+Video)

on

Mwanadada kutokea Kenya Vera Sidika amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii hasa hasa Afrika Mashariki baada ya kuamua kujibadilisha ngozi yake ya mwili na kuifanya nyeusi, Vera Sidika ambaye miaka kadhaa nyuma aliwahi kua na rangi nyeusi na baadae kufanya surgery na kuwa na rangi nyeupe.

Vera Sidika aliwahi kuthibitisha jambo hilo kupitia mahojiano aliyowahi kufanya nchini Kenya na kusema kuwa umbo la mwili wake hakuwahi kulibadilisha ndivyo alivyozaliwa lakini kwa upande wa rangi ya ngozi alibadilisha kutokana na kutovutiwa na rangi nyeusi kwa wakati huo na kujibadilisha kuwa mweupe.

Mchekeshaji Eric Omondi hakutaka hili la Vera Sidika kumpita aliamua kutumia ukurasa wake wa instagram kwa kupost video akiwa na Vera na kuandika caption inayosomeka “Amerudi, weusi ni dhahabu ukirudi kuwa mweusi karibu nyumbani”

AUDIO: MREMBO TUNDA NA WHOZU MAMBO HADHARANI “NIMECHAGUA LOVE SIO PESA”

Soma na hizi

Tupia Comments