Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Liverpool imecheza na Man United kwa mara 226 leo

on

Baada ya mapumziko za game za kimataifa za kirafiki zilizokuwa kwenye calendar ya FIFA weekend hii michezo ya ligi kuu England 2017/2018 iliendelea kama kawaida ambapo game kati ya Liverpool vs Man United ilipigwa Anfield.

Leo Jumamosi ya October 14 2017 Liverpool wamecheza na Man United kwa mara ya 226 huku Liverpool wakifanikiwa kuifunga Man United mara 75 na kupoteza mara 87 ambapo sare ya leo ya kutofungana (0-0) imefanya wafikishe sare ya 64 toka walipoanza kukutana April 28 1894.

Sare ya Liverpool vs Man United inaifanya Liverpool kuwa nafasi ya 7 katika msimamo wa Ligi Kuu England kwa kufikisha point 13 wakati Man United wapo nafasi ya pili kwa kufikisha jumla ya point 20.

ULIPITWA? List ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017

Soma na hizi

Tupia Comments