Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Chris Brown atambulisha ujio wake na Davido

on

Baada ya kuzagaa kwa picha nyingi kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha mkali wa RnB kutokea Marekani Chris Brown akiwa na Davido huku wengi wakijiuliza kama kuna matarajio ya ngoma mpya kutoka kwao sasa jibu ni hili hapa.

Chris Brown amedokeza kolabo yake na mkali huyo kutokea Nigeria Davido ambapo wimbo huo unaitwa “Blow My Mind” na Chris Brown ametujuza kuwa ngoma hiyo itatoka hivi karibuni. Kupitia ukurasa wa instagram wa CB ametuonyesha pia cover ya ngoma hiyo.


Davido aliwahi pia kufanya ngoma na rapper Meek Mill kwenye ‘Fans Mi’ iliyoachiwa rasmi June 5,2015 kupitia mtandao wa You Tube inaripotiwa kuwa Davido ameshaingia studio na kufanya ngoma mpya na wakali kutokea Marekani akiwemo mwimbaji/mwigizaji Ludacris, mtoto wa Diddy (King Combs) na mtayarishaji wa muziki Timberland. 

VIDEO: MTIKISIKO KWENYE MAPENZI YA MASTAA, ROMA, VANESSA, ALIKIBA, JE NI KWELI YAMEISHA?

Soma na hizi

Tupia Comments