Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

The weekend akerwa na ubaguzi wa rangi uliofanywa kwa mtoto wa Kiafrika

on

Staa wa muziki kutokea nchini Marekani “The Weekend” ambaye wengi walimfahamu zaidi baada ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa Selena Gomez amesikitishwa na kitendo cha brand ya nguo nchini humo H&MΒ kuwa wabaguzi wa rangi na kumdhalilisha mtoto mdogo.

Brand ya nguo ya H&M ambayo ni kubwa nchini Marekani imefanya tangazo na kumvalisha mtoto wa kiume mwenye asili ya Afrika nguo yenye maneno ya kumdhalilisha mtu mweusi yanayosomeka “Mimi ni nyani mtulivu msituni”

The weekend ameonyesha Β kukerwa na tabia walioifanya kampuni hiyo ya nguo ya H&M na kuamua kuandika kupitia ukurasa wake wa twitter na kusema kuwa hatofanya kazi tena na H&MΒ kutokana na kuwa wabaguzi wa rangi. Mastaa mbalimbali wamemuunga mkono The weekend akiwemo T.I na King Push

AUDIO:Alichoandika Jacquline Wolper baada ya Naibu Waziri kuita wasanii

Soma na hizi

Tupia Comments