Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Mshiriki wa Miss Tanzania kuhusu Deal alilosaini na kampuni ya PII

on

Baada ya mashindano ya miss Tanzania 2016 kumalizika hivi karibuni ambapo Fainali zake zilifanyika kwenye jiji la Mwanza kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo miaka zaidi ya ishirini iliyopita, Miss Tanzania 2016, Diana Lukumai aliitangazwa mshindi wa taji hilo.

Licha ya kutokuwa mmoja ya washiriki walioingia top ten, mrembo ambaye ni Miss Kilimanjaro, Glory Minja Leo November 3 2016 amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja kuwa balozi wa Kampuni ya Teknolojia ya Magari ‘PII’.

Akizungumza kuhusu mkataba huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Teknolojia ya Magari ‘PII’, Ebenezer Msuya amesema kampuni yao imeingia mkataba na Glory kutokana na uwezo ambao ameonyesha kwa kipindi ambacho walikuwa wakidhamini mashindano ya Miss Tanzania na baada ya kutambua uwezo wa washiriki hao walibaini kuwa Glory ana uwezo wa kufanya nao kazi.

>>>’Tumesaini naye mkataba wa kufanya kazi, leo tumemkabidhi cheque ya milioni lakini vilevile tumesaini naye mkataba wa mwaka mmoja ambao tutakuwa tunafanya nae shughuli za kijamii pamoja na shughuli nyingine za kimasoko’;- Msuya.

kulikuwa na vigezo walikuwa wanavihitaji mimi binafsi kuna vitu nilivifanya, walitupatia business card kwa kuwa walijua tutazunguka mikoa

Kwa upande wa Miss Kilimanjaro 2016 ambaye pia ni mshiriki wa Miss Tanzania, Glory Minja amesema ni nafasi ya kipekee kufanya kazi na kampuni hiyo ambayo imejikita zaidi katika teknolojia na atatumia nafasi aliyonayo katika jamii kuhakikisha anafanikisha malengo ambayo wanataka kuyafikia.

ULIKOSA HII MWANZO MWISHO KUHUSU FAINALI YA MISS TANZANIA 2016 MWANZA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement