Top Stories

Polisi watuhumiwa kuomba rushwa ya kreti za bia

on

Leo June 18, 2018 kuna hii kuifahamu Polisi nchini Uganda wanatuhumiwa kuwalazimisha wananchi wawanunulie kreti za bia kama namna ya kutoa rushwa ili waweze kuwaachia huru ndugu zao ambao wapo jela kwa kuvunja sheria za nchi.

Baadhi ya wakazi wamesema wamekuwa wakilazimishwa kufanya mambo nje ya sheria kutokana na kuwa na hamu ya kuwatoa ndugu zao waliofungwa jela.

“Hapa , kama polisi wakimkamata mtu, kitu cha kwanza wanachoomba ni kreti za bia kuanzia kreti 5 hadi 6 kabla ya kufikiria kumuachia ndugu yako” amesema Ms Lilian Andama Lawrence ambaye ni mkazi wa Offaka.

Wakazi hao wameyasema hayo mbele ya wafanyakazi wa Taasisi za Haki ya binadamu (FHRI), Freedom House na ”Judicial Service Commission” (JSC), ambao walitembelea eneo hilo.

Ms Sydey Etima-Ojara, ambaye ni msaidizi na mshauri wa chama cha JSC na Ms Maria Kaddu Busuulwa ambaye Mwenyekiti wa Taasisi ya Haki na sheria wa FHRI wamesema kuwa wanahitaji kuwaelimisha wakazi juu ya kukataa kutoa rushwa inayoombwa na polisi hao.

Ameongezea kuwa kufuatia tukio hili kuna uhitaji mkubwa wa kuwasimamia vyema polisi ili kudhibiti vitendo hivyo.

LIVE MAGAZETI: Zitto: Bajeti inatia shaka, Basi la Mbunge Msukuma lauwa watano

 

Soma na hizi

Tupia Comments