Top Stories

Lugola “Mashoga wapo salama nchini, anaetishwa aende Polisi”

on

Leo November 7, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kangi Lugola amesema kuwa wapenzi wa jinsia moja hawapo hatarini nchini humo.

Lugola amesema japo ushoga ni kosa la jinai nchini Tanzania, wanaojihusha na vitendo hivyo hawatishiwi maisha na wala hawaikimbii nchi.

Akizungumza na gazeti la serikali la Habari Leo, Lugola amekanusha kuwa wapenzi wa jinsia moja wapo hatarini.

“Ninachosema ni kuwa Tanzania ni salama na hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kuwa sio salama bila ya kuwa na vigezo husika, kama mtu yeyyote anahatarishiwa maisha yake, basi napaswa kwenda polisi na mimi sijapata taarifa zozote kutoka polisi zinazoeleza kuwapo kwa mazingira hatarishi ya watu hao,” Lugola 

Siri ya Makonda kukimbilia Kanisani katika vita ya Dawa za Kulevya na Ushoga

Soma na hizi

Tupia Comments