Tangaza Hapa Ad

Michezo

Ushindi wa Simba unaowafanya wakutane na Yanga nusu fainali Mapinduzi Cup 2017

on

Baada ya jana January 7 2017 Dar es Salaam Young Africans kuruhusu kufungwa goli 4-0 dhidi ya Azam FC na kumaliza Kundi B wakiwa nafasi ya pili, Simba wameifunga Jang’ombe Boys goli 2-0 na kuifanya Simba kumaliza Kundi A wakiwa nafasi ya kwanza.

Ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys zilizofungwa na Laudit Mavugo dakika ya 12 na 54, imeifanya Simba kumaliza nafasi ya kwanza katika msimamo wa Kundi A wakiwa na point 10, kwa mujibu wa mashindano haya ni kuwa mshindi wa kwanza wa Kundi A (Simba) atacheza na mshindi wa pili wa Kundi B (Yanga), mchezo huo  wa nusu fainali utachezwa Jumanne ya January 10 saa 20:15 usiku.

Kwa maana hiyo Azam FC waliyokuwa vinara wa Kundi B kwa jumla ya point saba wanausubiri mchezo wa mwisho wa Kundi A kati ya URA ya Uganda ambao ni Mabingwa watetezi dhidi ya Taifa Jang’ombe ili kuweza kufahamu atacheza na nani katika hatua ya nusu fainali ya Mapinduzi Cup 2017.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Tupia Comments

Advertisement