Premier Bet

Top Stories

DC Sabaya alivyobeba mfuko wa cement kichwani, amuonya Kamanda “nitakushughulikia” (+video)

on

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amekabidhi mifuko ya saruji 200 na nondo tani moja pamoja na kokoto lori moja kwa Kituo cha Polisi cha Boma Ng’ombe Wilayani Hai kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.

Akikabidhi vifaa hivyo vya ujenzi Lengai Ole Sabaya amemtaka Kamanda wa Polisi wa Wilaya Lwelwe Mpina kusimamia vizuri matumizi ya vifaa hivyo vya ujenzi hivyo alivyo vitoa kwa jeshi hilo.

“Nimeleta makusudi mifuko 200 ya cement, nondo piece 100 ili kupanua Kituo cha Polisi cha Boma Ng’ombe hiyo itawarahisishia Wananchi kupata huduma kwa haraka, ndani miezi mitatu jengo litaisha, OCD sitegemei mfuko hata mmoja upotee” DC Hai Lengai Ole Sabaya

IKULU: RAIS MAGUFULI LEO AMEMTEUA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

Soma na hizi

Tupia Comments