Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Beyonce aingiza mabilioni ya pesa kupitia kampuni ya Uber

on

Mtandao wa Complex umeripoti kuwa mwimbaji Beyonce ameingiza kiasi cha dola za Kimarekani Mil. 300 sawa na zaidi ya Tsh. Billioni 691 za Kitanzania kutoka UBER kwenye uwekezaji wake wa muda mrefu. Wiki iliyopita kampuni hiyo ya Usafiri ilitangaza kuingiza faida za hisa zake kiasi cha dola 8.1 Billioni sawa na Trilioni 18 za Kitanzania.

Inaripotiwa kuwa mwaka 2015 kampuni ya Uber ilimpatia Beyonce dili la kutumbuiza kwenye moja ya Events zao kwa kiasi cha Dola Millioni 6 za Kimarekani sawa na zaidi ya Tsh bilioni 13 za Kitanzania na badala yake Beyonce aliwaomba wampatie pesa hizo kwa njia ya hisa na kwa sasa inaripotiwa kuwa hisa zake kwa sasa zinaweza kununuliwa na mtu yoyote.

Beyonce sio staa pekee ambaye ameingiza pesa nyingi kupitia kampuni ya Uber, inaelezwa kuwa Jay Z pia ana hisa kwenye kampuni hiyo, ikiwemo muigizaji Leonardo di Caprio, Ashton Kutcher , Olivia Munn na Jeff Bezos wa Amazon.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MIMI MARS KUZUNGUMZA KUHUSU YEYE NA PERFECT NI WAPENZI..? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments