Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

U HEARD: Masizi yamtibua Barakah Da Prince kwenye Video Cover ya Stan Bakora

on

October 10, 2016 Baada ya kuachiwa kwa Video ya wimbo Nisamehe wa msanii Barakah Da Prince aliompa Collabo Star wa single ya Aje Alikiba, Headlines mpya zimeibuka tena kutoka kwa mchekeshaji Stan Bakora aliyeamua kuifanya Cover ya Video hiyo.

Kupitia U Heard ya Clouds FM, Mtangazaji Soudy Brown amepiga story na Baraka Da Prince aliyeonekana kukerwa na jinsi Stan Bakora aliyeamua kujipaka Masizi usoni ili kufanana na Rangi ya msanii huyo na kwa mujibu wa Stan Bakora amedai kwamba anamshangaa Barakah kwasababu walikubaliana kila kitu ila ameshangaa kuona akimuandika vibaya Instagram.

>>>Yule mtoto namuona kama mshamba ujue kwasababu tabia hizo anazo sana halafu dah tulikubaliana nikamwambia mimi nataka niifanye Cover akasema fresh tukamalizana sasa mwisho wa siku anaanza kuropoka wakati alitakiwa kusema bwana tulikubaliana ufanye cover yangu lakini hapa kuna hiki na hiki sijapenda we unakwenda kuandika kwenye page yako unadhani watu wananichukuliaje mimi? – Stan Bakora.

>>>Stan alinipigia simu akaniomba kufanya video cover ya wimbo wangu nikamwambia wasiliana na management yangu sasa sijui walikubaliana nini na Aidan (Manager wa Barakah) sikutaka kufatilia waliongea nini ila baada ya muda nikaona hiyo video. Mi sijapenda yale masizi aliyopaka ni kama anaikashifu rangi yangu, mi najipenda nilivyo na sipendi mtu anikashifu ndio mana nikamchana:- Barakah Da Prince.

ULIMISS KUMUONA VANESSA MDEE AKIPERFORM KWENYE CONCERT MOMBASA KENYA? TAZAMA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement