Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu nae kapata timu Ulaya

on

Baada ya kumalizana kimkataba na timu ya TP Mazembe ya Congo DRC mwishoni mwa mwaka 2016 na kutotaka kuongeza mkataba kwa madai ya kuwa anaenda kucheza soka Ulaya, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu amepata timu ya kucheza Sweden na tayari amesaini mkataba wa kuitumikia.

Thomas Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu ya inayoshiriki Ligi Kuu Sweden inayoshirikisha timu 16 ambapo kwenye Interview na shaffihdauda.co.tz Ulimwengu amethibitisha dili hilo kukamilika na kwa sasa anasubiri VISA tu.

 “Kweli nimesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo ambayo nitajiunga nayo hivi karibuni, kwa sasa nashughulikia mambo ya visa na taratibu nyingine, kuanzia wiki ijayo  nitakuwa nimeshajiunga na timu ya Athletic Football Club Eskilstuna  ya Sweden”
ULIPITWA?: Mtazamo wa Thomas Ulimwengu kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi ya Tanzania, BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement