Duniani

Mwanaume aliyevua condom akiwa mapenzini ahukumiwa kwenda jela

on

Mwanaume mmoja ambaye ametajwa kuwa ni raia wa Ufaransa kwenye taifa la Switzerland amehukumiwa kwenda jela miezi 12 baada ya mpenzi wake kumshtaki kutokana na kuivua kinga ‘Condom’ wakiwa mapenzini. 

Mwanamke alisimulia kuwa walianza kufanya tendo la ndoa wakiwa na kinga na walipomaliza mwanamke aligundua kinga imevuliwa kinyume na matakwa yake hivyo alitoa taarifa hiyo polisi, Mwanaume huyo alikamatwa na baadae kufikishwa mahakamani na akashtakiwa kwa ubakaji.

Akiwa mahakamani mwanaume huyo alidai kuwa lengo lake lilikuwa ni kuvaa kinga lakini ilipasuka. Mwanamke alisisitiza kuwa angejua jamaa hatumii kinga asingekubali kufanya tendo hilo, Mwanaume huyo amefungwa jela miezi 12 lakini ameonyesha nia ya kukata rufaa

VIDEO: ‘Nimeshawahi kwenda kwa Mganga wa kienyeji’ – Darassa, Bonyeza play hapa chini kutazama

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments