fB insta twitter

Ok ok!! tunajua Peter Msechu karudia wimbo wa Ben Pol, Salama Jabir kasemaje? Ben Pol mwenyewe imebidi aongee hapa

on

Msechu 1Kwenye playlist ya Radio za Tanzania sasa hivi kunayo single ya Sophia pia ambayo original yake imefanywa na Ben Pol lakini Peter Msechu kaifanyia kazi na kuitoa remix yake.

Kama ulikua hujui, haya ndio maneno ya Ben Pol baada ya Peter Msechu kuirudia >>>Kiukweli mimi nimependa sana na alinitumia, unajua hivi vitu ni lazima mtu anakushirikisha sababu wewe umetunga, una producer wako, manager wako…….. nimependa sana kuliko labda nyimbo ingetoka unakutana nayo

Msechu alinipigia simu akaniambia, niliona hii ni heshima kubwa sana na Msechu ni miongoni mwa ninaowakubali, nimeisikiliza single nimedata, Mswaki Producer wangu pia nae kadata, tunaisikiliza kila saa…. ni kazi flani nzuri sana, mpaka leo Mswaki ametoa wazo kwamba au tutoe beat chorus kwa mtu anaetaka kufanya? mbona kama imekua inavutia?‘ – Ben Pol
Maneno ya Ben Pol unaweza kuyasikiliza hapa chini pia pamoja na hiyo single aliyorudia Msechu.


Ben ameongeza saa kadhaa tu baada ya mtangazaji maarufu wa TV Salama Jabir kuguswa na alichofanya Msechu na kuyaandika haya yafuatayo kwenye page yake ya twitter.

Msechu kapatia kwa asilimia ngapi kama umeisikiliza remix?

Salama

Soma na hizi

Tupia Comments