Michezo

Bado mambo sio mazuri FC Barcelona wamekubali kipigo tena leo April 17 2016 (+Video)

on

April 17 2016 Ligi Kuu Hispania iliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali, mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Valencia ndio ulikuwa wa kuvutia zaidi kwani mashabiki wa soka walikuwa wana hamu ya kufahamu kama FC Barcelona atakubali kipigo tena Nou Camp baada ya kufungwa na Madrid April 2.

Bado mambo sio mazuri kwa FC Barcelona leo April 17 2016 wamekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Valencia katika uwanja wao wa Nou Camp, hivyo hilo ni pigo tena baada ya siku chache tu zimepita toka waondolewe katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Atletico Madrid.

3347267600000578-0-image-a-1_1460921203091

Valencia walianza kufunga goli dakika ya 26 kupitia kwa mchezaji wa FC Barcelona Ivan Rakitic kujifunga, goli ambalo liliwafanya FC Barcelona kuhangaika kusawazisha ila Valencia wakafunga goli la pili dakika ya 45 kupitia kwa  Santi Mina ila Lionel Messi dakika ya 63 aliipatia FC Barcelona goli la kufutia machozi.

Kwa matokeo hayo FC Barcelona ambao awali walikuwa wameziacha timu za Atletico Madrid na Real Madrid kwa point zaidi ya 5, wametoa nafasi ya nafasi ya kuwania Ubingwa kwa timu hizo kwani FC Barcelona anaongoza Ligi kwa tofauti ya magoli akiwa na point 76 sawa na Atletico, huku Real Madrid wakiwa na point 75.

Video ya magoli ya FC Barcelona vs Valencia, Full Time 1-2

https://youtu.be/HZAL9Cg11-Y

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

VIDEO YA GOLI LA NNE LA MBWANA SAMATTA AKIWA NA KRC GENK YA UBELGIJI

Soma na hizi

Tupia Comments