Mmiliki wa studio ya Free Nation, Mr T Touch ambaye ana list ya ngoma kali zinazosumbua sana kwenye chati ya muziki kumbe nae ana ngoma ambazo anasikiliza na ambazo hazisikilizi kabisa!
Kwenye zile anazozisikiliza kwa sasa iko ya Darasa pamoja na wimbo wa Godzilla ‘Nobody’.
T Touch amesema alitamani sana kufanya kazi na Godzilla, anafurahia kuliffanikisha hilo kwa sasa.
Baada ya msanii Afande Sele kutangaza kugombea Ubunge hivi karibuni kupitia chama cha ACT, kumekuwa na maswali mengi moja ni hili; eti akipata Ubunge atakata rasta zake?
Akizungumzia ishu hiyo kwenye 255, Afande Sele amesema inategemea na Katiba inasemaje.. anachokiona ni kwamba wapo Wabunge masingasinga ambao wanafunga vitambaa na kuingia Bungeni bila tatizo, yeye atakuwa Mbunge wa kwanza mwenye rasta jambo ambalo litawafurahisha na kuwashangaza watu wengi.
Wasikilize wenyewe hapa Afande Sele na T Touch.. Hii nimekusogezea kutoka #255 @CloudsFM
millardayo.com ndio sehemu utakayozipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook