Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Kwenye 255 ya leo Feb 16, amesikika Ben Pol, Dully Sykes na TID. Yote iko hapa (Sauti)

on

ben paul

Ben Pol

Kwenye 255 ya leo February 16, story ya kwanza kusikika inamhusu msanii Ben Pol ambaey amezungumzia mpango wake wa kufanya video ya wimbo wake wa Sofia mkoani Dodoma na kusema kuwa, uamuzi huo umetokana na ujumbe ambao uko kwenye wimbo huo ambao unahitaji mazingira ya uhalisia zaidi yanayopatikana mkoani humo.

maxresdefault

Dully Sykes

Baada ya taarifa za msiba wa baba mzazi wa msanii Dully Sykes mzee Ebby Sykes, Dully amesema kuwa kifo cha baba yake kimetokana na matatizo ya vidonda katika miguu yake na kupelekea kifo chake kilichotokea wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mazishi yake yatafanyika leo katika makaburi ya Kisutu.

Msanii TID ambaye marehemu mzee Sykes alishiriki kupiga gitaa kwenye wimbo wake wa Aisha, amesema kuwa Mzee Sykes alikuwa baba ambaye alipenda kuona watoto wake wakifurahia maisha na amefanya nae show nyingi kwa kupiga gitaa na alikuwa na mpango wa kufanya nae wimbo.

ebby

Marehemu Ebby Sykes, baba mzazi wa Dully Sykes

Bonyeza play kuweza kuisikiliza 255 yote hapa.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram,  na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments