Habari za Mastaa

Za kwenye 255 leo FEB17, yuko Nikki wa Pili kutoka WEUSI, AT na Madee.. (Audio)

on

Niki wa Pili

Nikki wa Pili

Jumanne ya February 17, story ya kwanza kusikika kwenye 255 inamhusu msanii Nikki wa Piliamezungumzia ishu ya wimbo wake wa Safari kuongoza kwa kusikilizwa na mashabiki wake wa Mtwara.

Nikki wa Pili amesema kituo kimoja cha Radio Mtwara hufanya tathmini kwa kila wiki kwa kutembelea sehemu mbalimbali wanazo-burn CD ambapo wimbo wake wa Safari ndio uliongoza  kwa ku-burn , kuwekwa kwenye simu na kuombwa kwenye playlist.

Nikki anaamini kwamba hiyo inatokana na wimbo huo kuwa na mashairi mepesi na unaoeleweka.

AT 2

AT

Mwaka jana kuna mganga ambaye alijitokeza akafungua kesi kwamba anamdai pesa msanii AT kutokana na tiba aliyomfanyia, AT amesema kuwa alishinda kesi hiyo kutokana na kukosekana kwa ushahidi suala ambalo lilimuathiri sana kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote, hii kwake ni changamoto kwani yeye anafanya muziki kwa kumtegemea mwenyezi Mungu.

DSC_0787Msanii Madee amesema video ya Vuvula ambayo ilizinduliwa siku chache zilizopita haijatoka kwa sababu kuna vitu vilifanya wachelewe kuitoa ikiwemo maneno yaliyoanza kusemwa kuhusu ile teaser ya wimbo huo iliyotoka siku chache kabla ya uzinduzi.

Madee amesema kutakuwa na video mbili za wimbo huo, moja itapatikana kwenye mtandao na nyingine kwenye vituo vya television.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments