Mix

Mambo 13 Nchi za Kiarabu zimeitaka Qatar itekeleze…moja ndani ya siku 10

on

Mtandao wa AL JAZEERA umeripoti leo June 23, 2017 kuwa nchi nne za kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia zimeipa Qatar masharti 13 ili kumaliza mgogoro uliopo baina yao ambapo moja katika masharti hayo ni kuitaka kukatisha mtandao wa Al Jazeera na kupunguza mahusiano na Iran.

Pia katika list hiyo, mataifa hayo yameitaka Qatar kutokuwa na mahusiano pia na makundi ya Muslim Brotherhood, Hezbollah, al-Qaeda na ISIL (pia hujulikana kama ISIS) wakiitaka pia kufunga kambi moja ya wanajeshi ya Uturuki ndani ya kipindi cha siku 10 pekee.

Nchi za Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu na Bahrain zilisitisha uhusiano wa kidiplomasia na Qatar mwezi huu kwa madai kuwa nchi hiyo inafadhili Ugaidi – madai ambayo Qatar inayapinga.

“Hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni” – Rais Magufuli!!!!

Soma na hizi

Tupia Comments