Nguli wa masuala ya Fashion Duniani na Mzaliwa wa Ujerumani Karl Lagerfeld amefariki leo February 19,2019 Jijini Paris akiwa na umri wa miaka 85, Karl maarufu kama ‘Kaiser’ ni mmoja wa Watu ambao wapo nyuma ya pazia wa mafanikio ya brands za Tommy Hilfiger, Chanel na Fendi.
Mwaka 1980 Karl alikuwa maarufu kupitia fashion duniani kote na alipendwa na watu wengi kutokana na ubunifu aliokuwa akionyesha katika maisha ya uwanamitindo na alijizolea umaarufu pia baada ya kuonekana kubadilisha kampuni kila mara.
Kupitia mwaka huo huo 1980 aliweza kurudisha kampuni ya Chanel kwenye soko baada ya kampuni hiyo kuyumba na kupoteza muelekeo na ndipo baadhi ya watu walipooanza kununua bidhaa kutoka kwenye kampuni hiyo ya Chanel.
VIDEO:FLORA KAONGEA BAADA YA KUDAIWA KUMTOROSHA PASCAL WA BSS HOSPITALI