Hawa jamaa wawili wanaoonekana kwenye picha walikua ni sehemu ya timu ya Nicki Minaj, walikwenda sehemu inaitwa Philadelphia Marekani ambapo ni siku mbili tu zimepita toka waingie kwenye mji huo kwa ajili kujiandaa na ziara ya kimuziki ya Nicki Minaj.
Polisi wamesema aliyefariki ni De’Von Pickett, 29, au Day Day anaeonekana kushoto kwenye picha Eric Parker, 27 mwingine aliyejeruhiwa anaendelea vizuri na matibabu.
Kilichotokea ni wao kuchomwa visu kwenye ugomvi uliotokea wakiwa Baa usiku wa Jumanne na rafiki zao ambapo baada ya kuchomwa visu walikimbizwa Hospitali lakini muda mfupi baadae Day Day akawa amefariki.
Polisi wamesema watamzawadia milioni zaidi ya thelathini na tano mtu yeyote atakaefanikisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa aliewachoma visu.
Two members of my team were stabbed last night in Philly. One was killed. They had only been there for two days rehearsing for the tour.
— NICKI MINAJ (@NICKIMINAJ) February 18, 2015
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook