Habari za Mastaa

966 ya Nay wa Mitego haijaishia kwenye magari na nyimbo tu,imefika huku sasa hivi…

on

Nay-wa-mitegoNamba 966 licha ya kuwa ni namba ya kawaida kama namba zingine lakini ni namba ambazo Msanii wa Tanzania Nay wa Mitego ameamua kuzitumia yeye rasmi kama namba zake muhimu kwake kwenye baadhi ya vitu vyake.

nayU-serious wa namba hizi kwa Nay ulianzia kwenye nyimbo zake ambapo amekua akizitaja mara kwa mara baadae tukaanza kuziona kwenye magari yake kumbe hazijaishia hapo kwa sasa Nay anasema hata document muhimu kama TIN namba zake zina namba hii.

Screen-Shot-2014-09-06-at-9.46.47-PMIngawa bado hajataka kuweka wazi kuhusu namba hizi licha ya kujua kuwa kachanganya tarehe,mwezi na mwaka aliozaliwa inawezekana ana sababu nyingine,Nay kaongea na millardayo.com na kusema>>’Kwa sasa hata baadhi ya vitu vyangu nasajili kwa namba hiyo hata Tin namba yangu niliomba nikapewa hiyo so ni namba ambazo zimeshakua rasmi kwangu’

Swali lingine millardayo.com ilitaka kufahamu inakuaje pale anapoagiza Gari halafu haijafika hiyo namba>>’Huwa nasubiri kwa sababu huwa natoa oda na nahitaji hizo namba so naambiwa mpaka zifike ni muda fulani huwa nasubiri kwa mfano hii Hiace ya watoto wangu kuendea shule imekaa muda bila kuwa na namba mpaka imekuja kupata namba juzi’

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments