Muigizaji wa kiume anaefanya vizuri katika tasnia ya Bongo Movie Tanzania, Rammy Galis leo November 18 2016 anatusogezea story kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na mrembo Agnes Masogange ambapo inadaiwa mapenzi yao yamevunjika, na zile ishu za kutopostiana katika mitandao ya kijamii hazipo tena.
Rammy ameongea na AyoTV na millardayo.com ambapo ameyaungumza haya…….>>>“Unajua mahusiano ni mahusiano tu, hakuna lenye mwanzo linakosa mwisho hakika yale yalikua ni mahusiano na hakika yamefika mwisho, kwa hiyo sidhani kama nina jambo la zaidi la kulizungumzia zaidi ya hilo siwezi nikaweka tofauti zetu hadharani, ilikuwa ni mahusiano na yameishia.” – Rammy Galis
VIDEO: Kama ulipitwa na hii, nimekuwekea hapa sababu za Dokta Cheni kuacha kuigiza