Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo February 8 2017 amesimama mbele ya Waandishi wa habari kwenye awamu ya pili ya ishu ya dawa za kulevya na kutaja watu mbalimbali wanaotakiwa kufika Polisi Ijumaa kwa ajili ya mahojiano kuhusu ishu za dawa za kulevya.
Kabla ya kuhitaja List hiyo ya wa tu 65, RC Makonda ameeleza njia 5 ambazo zinatumika na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, baada ya kufanya utafiti wake…….
- Watu wananunua dawa kutoka Pakstani wanakuja na meli, meli inapakia mizigo, meli ikishapaki mzigo wanachukua dawa za kulevya wanaingiza kwenye mifuko kama ya sukari halafu wanapakia kwenye mapipa wanayaingiza kwenye meli, meli zinapokuja zinapokaribia kwenye bandari zetu wanayatupa mapipa hayo yakiwa yamefungwa na GPRS, maeneo wanayoyatupa mapipa hayo ni Zanzibar, Tanga na Bagamoyo. wakishakuja kwenye bandari zetu hawana dawa za kulevya baadye timu inaenda wakiwa na boti wakiwa na mashine zao za kusoma GPRS wananyanyua yale mapipa.
- Njia ya magari, mtu ananunua magari Japan lakini hatoki moja kwa moja Japan kuja Tanzania anapita nchi zingine kwa ajili kuweka mzigo, anafungua baadhi ya sehemu a magari wanaweka dawa za kulevya.
- Watu wanafanyabiashara kwenye meli za mafuta, sisi huwa tu tunaangalia mafuta kama yana viwango sasa huwa wanatumia huo mfumo kusafirisha
- Kuna watu wana sehemu zao za kupack boti zao hawaingiliwi na mtu, anachokifanya anaenda kuchukua mzigo anasafirisha.
- Kuna wanaotoa dawa za kulevya hapa kwa mfano kuna mama ambaye kazi yake ni kusafirisha watoto wa kike anasema anaenda China kununua bidhaa, anasafirisha watoto wa kike wenye umri wa kati, wanapewa dawa wanasafiri nazo wanapewa na Dola 5000 akifanikiwa kuingiza analipwa dola 7,000
Ulikosa? maagizo matatu ya Paul Makonda aliyayatoa Feb 6 2017, Bonyeza play hapa chini