Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi kutumika kwa namna yoyote ile wimbo ‘WAPO’ uliombwa na msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego.
Kwa mujibu wa BASATA, kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kusimami kazi za Sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yafanyikayo katika tasnia ya Sanaa hayaachi taifa na wasanii katika hali zisizokuwa salama.
Katika kutekeleza majukumu haya, Baraza linahakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi zozote za sanaa.
Wakati huo huo, BASATA linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa nchini kuzingatia ubunifu wa hali ya juu kufanya kazi za Sanaa ili kuweza kufikisha jumbe mbalimbali za kufundisha, kuelemisha, kuburudisha na kuonya.
Kadhalika, Baraza linawaonya wote wanaozitumia kazi zilizopigwa marufuku. Ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi ambapo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
ULIIKOSA HII YA POLISI MOROGORO KUHUSU KUMKAMATA NAY WA MITEGO? BASI BONYEZA PLAY KUMSIKILIZA KAMANDA WA POLISI MATEI KWA UFAFANUZI ZAIDI.