Mastaa Chege na Temba ni kati ya wasanii waliodumu kwa muda mrefu kwenye Bongofleva wakifanya vizuri hata nje ya mipaka ya Tanzania ambapo hivi karibuni wameachia wimbo wa ‘Go down’ unaofanya vizuri kwenye chart mbalimbali za muziki.
Licha ya wimbo wa Go down kupendwa sana mashabiki wao, lakini wengi hawaijui maana halisi ya wimbo huo na kwa kulifahamu hilo, usiku wa April 14 2017 kupitia The Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chege ameeleza maana halisi iliyobeba wimbo huo huku akisema haumuongelei mtu wala upepo wa siasa uliopo, bali ni ngoma ya Chege na Temba ambayo haihusiani na maisha ya mtu binafsi bali jamii.
>>>”Ile ngoma ni kwa watu wote ambao wanaongea sana, so, Go down haihusiani na siasa, ni ngoma ya mapenzi. Haihusiani na maisha yangu, ni ngoma ya Chege na Temba inayozungumzia jamii na siyo mtu binafsi.” – Chege.
Chege pia amegusia sababu za kukaa muda mrefu bila kufanya kazi ya pamoja na Temba na kugusia gharama za show zao akisema:>>>”Ni kweli mashabiki wamewazoea Chege na Temba kwa muda mrefu. Kwa hiyo, muda mwingine wakimuona Chege peke yake au Temba peke yake, wanaona kuna vitu fulani vinapungua. Tulijipanga kwa muda mchache kwa sababu watu walikuwa wanaulizia Chege na Temba takaamua kufanya.
“Simu za Promoter zimeshalia nyingi tu zikituhitaji tufanye show japo suala la kujua ni Shilingi ngapi, hilo ongea na Mkubwa Fella. Hata nikipokea simu ya mtu yeyote namtupa kwa Fella. Hatujawai kugombana na Temba na ikitokea mara nyingi Temba ananiambiaga Go down maana mimi mtata kidogo.” – Chege.
VIDEO: Harmorapa amezungumzia lugha kwenye collabo na msanii wa nje