Siku chache baada ya kuachiwa wimbo mpya ‘Cheche’ kisha kuibuka story za mtu wingine aliyefahamika kwa jina la Modala kudai wimbo huo ni wake, mwimbaji Ommy Dimpozi amesisitiza kuwa wimbo huo ni haki yake.
Akizungumza kwenye The weekend Chat Show ya Clouds TV Ommy Dimpoz amesema kuwa wimbo huo aliandikiwa na watu wenye maamlaka na kusema yeye pekee ndiye ana haki nao akisema kwa sasa hamlaumu mtu yeyote na halalamiki.
>>>“Nina haki na huu wimbo siyo wa mdomo tu hata kwenye makaratasi. Kwa hiyo siwezi kulaumu wala kuongea kwa yule msanii anayelalamika au kusema kwamba dogo anazingua, no.
“Sijui, labda ni kitu gani maana hata mimi imebidi niulize mbona kuna msanii analalamika? Jamaa akanijibu kama kuna mtu yeyote anakuuliza hilo suala sisi tuna majibu wewe waambie watutafute, so, siwezi kuongelea chochote kuhusu Modala.
“Siwezi kusema sana kama ni mtu katumwa, katengenezwa au nini ila pia unajua muziki una mambo mengi. Hayo mambo yanaweza kutokea ila siwezi kumshutumu mtu yeyote. Pengine unaweza kumlalamikia kwamba huyu dogo katumwa wakati na yeye ana haki na huo wimbo ila majibu wanayo wao walioandika.” – Ommy Dimpoz.
“Wimbo wa Ommy Dimpoz ni mali yangu ila…” – Producer Abydaddy
ULIPITYWA? Alichoongea Ommy Dimpoz aongea baada ya kusainiwa Rockstar4000!!!