Baada ya muda mrefu kupita tangu kuwepo taarifa kuwa serikali ya Tanzania na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA zingekutana kwaajili ya mazungumzo, hatimaye ACACIA leo wametoa taarifa kuwa wataanza kulipa kodi ya mrahaba ya 6% bada ya 4% ilikuwa ikilipwa awali.
Pia kampuni hiyo imesema kuwa italipia 1% nyingine kwenye hatua za ukaguzi wakati wa usafirishaji wa madini yote yatakayokuwa kwenye makontena ya makinikia.
Kampuni ya uchimbaji madini ACACIA imekubali kulipa nyongeza ya mrahaba wa 6% kutoka 4% ya mwanzo, pia italipia 1% kwenye hatua za ukaguzi. pic.twitter.com/QyitYYDBN3
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
VIDEO: Umepitwa na uchambuzi wa Magazeti ya leo July 14, 2017? Bonyeza play kutazama hapa chini