Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.
Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.
Aidha, sababu aliyoitumja Jaji Lugano ni kutokuwepo kwa kifungu sahihi ambapo kunayafanya maombi hayo yasiwe sahihi Mahakamani.
#BREAKING: Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 waliofutwa CUF kutaka Wabunge wateule wasiapishwe na Bunge.
— millardayo (@millardayo) August 4, 2017
Play kwenye video hii kushuhudia Wanachama wa CUF walivyopigana ndani ya Mahakama Kuu…