Siku kadhaa zilizopita kupitia millardayo.com kuna taarifa zilitoka kuhusu kufungiwa kwa video ya Jux ambayo haijaonyeshwa kwenye TV za Tanzania siku kadhaa tu baada ya kutoka.
Stori nyingine ikafata kuhusu kufungiwa kwa video ya ‘nimevurugwa’ ya Snura, taarifa ambazo zilitolewa na meneja wa wake ambae ni ‘HK’ akidai sababu maalum bado hawajazipata ingawa kila kituo cha TV anachokwenda wanampa sababu tofauti.
millardayo.com haikuishia hapo ilienda moja kwa moja kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ili kuujua undani wa hii ishu.
Kutoka Basata huyu ni Godfrey Mungeleza, kaimu katibu mtendaji anasema >> ‘unaposema kufungia video mojakwamoja kuna chombo kingine cha serikali kinashughulikia hilo ambao ni bodi ya filamu Tanzania’
‘Bodi ya filamu wanaangalia video zote, wanapoona hii haikidhi au haifai kwa jamii za Kitanzania basi wanaisimamisha kidogo wanamshauri aweze kuirekebisha ili iweze kulingana na maadili ya kitanzania, sisi tunaangalia audio kabla haijaingia sokoni katika urasimishaji tunakaa tunausikiliza muziki wake tunashauriana kwamba akarekebishe hapa na tunaangalia mambo mengi ikiwemo ubunifu wake mwenyewe’
‘Suala la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la maadili na limeandikwa sana na sisi kama Baraza tunaangalia sana suala la maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia msanii mwenyewe’