Habari za Mastaa

Chris Brown na Miley Cyrus waipa shavu Kenya

on

cccObama, Rupita Nyong’o na wanariadha mbalimbali wameipa jina kubwa Kenya kwenye nchi mbalimbali duniani na kuendelea kujulikana na zaidi.

Chris Brown anamiliki clothing line ambayo inaitwa Black Pyramid na ameshatoa nguo za aina mbalimbali kama T shirts,kofia,hoods na vingine.

Kwenye nguo zake mpya ambazo ni Black Pyramid International zina bendera za nchi mbalimbali kutoka kwenye kila bara duniani ili kukamilisha title ya Black Pyramid International.

Chris Brown amechagua bendera za mataifa makubwa kama kwao Marekani,Ujerumani,Brazil,U.K,Japan na kutoka Africa ameichagua Kenya peke yake.

kenya

Miley Cyrus ambaye jina lake lilitafutwa sana kwenye Google mwaka jana kutokana performance yake na Robin Thicke amesema ana ndoto kubwa ya kutembelea Kenya.

Miley akiongea kwenye interview na New York Observer alisema kwamba huwa hatoki sana nyumbani kwake kwasababu ana kila kitu anachokita hapo nyumbani.

Huwa haendi kwenye movie theater kwasababu ana TV kubwa sana nyumbani, hapendi kwenda kula restaurant kwasababu ana mpishi mzuri nyumbani lakini ana ndoto kubwa ya kutembelea Kenya.

“I want to go to Kenya, Kenya is my dream,” she says. “Kenya is my total dream. I wish I wasn’t going to be in Minneapolis next week, I wish I could be in Kenya.”- alisema Miley

Tupia Comments