Wiki mbili zimepita tokea muigizaji Munalove ampumzishe mwanae Patrick katika nyumba yake ya milele na hivyo leo July 18,2018 kwa mara ya kwanza amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mwanae pamoja na baba mzazi wa Marehemu Patrick.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Shilole ameonyeshwa kuchukizwa na kitendo alichokifanya Munalove cha kuita na kuzungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa hajawahi kuona mwanamke kama Muna
“Hakuna siku nimevurugwa kama Leo, hakuna mwanamke wa namna hii kwenye hii Dunia!!! Sijawahi kuona mwanamke mwenye roho ngumu kwenye hii Dunia kama munah!!..😢😢😢😢#YouGirlUtapataTabuSanaaaa!!!”
BREAKING LIVE: Muna Love anafunguka “Nitaendelea kusema ukweli Baba yake Patrick ni Casto”