Ikufikie hii story kuhusiana na Mwanasheria wa msanii R.Kelly ambaye ameomba kujitoa kwenye kesi inayomkabili msanii huyo baada ya kutuhumiwa kuingilia mapenzi kati ya mke wa mtu na kuivunja ndoa hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa mwanasheria huyo M.Craig Robertson aliandika barua kwa Jaji Mkuu ya kujitoa kwenye kesi hiyo na kumtaka R.Kelly kutafuta mwanasheria mwingine.
Mkazi wa mji wa Mississippi Kenny Bryant anamshtaki msanii huyo wa RnB R.Kelly kuivunja ndoa yake kwa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mke wake, inaelezwa kuwa sheria za mji huo zinaruhusu mtu kushtaki kama akivunjiwa ndoa yake.
PANCHO ALIVYOAGWA DSM: LAMAR, LIL OMMY, MONA GANSTAR WAMEZUNGUMZA