Licha ya kwamba watu mitandaoni wamelipokea tofauti swala la Wema Sepetu kuomba msamaha mbele ya vyombo vya habari baada ya video yake fupi iliyosambaa akikiss na mwanaume anayeaminika kuwa ni mume wake mtayarajiwa siku kadhaa zilizopita.
Ombi la Wema Sepetu limeonekana kuwa tofauti zaidi kwa msanii mkongwe Ray C kwani yeye ameonyesha kukubali kumsamehe Wema Sepetu kutokana na kosa lake alilolifanya na kuamini kuwa bado anayo nafasi ya kufanya vitu vingine upya.
Kupitia ukurasa wa instagram Ray C ameandika “Nakumbuka 2006 Mange alinipigia Simu akaniambia anakuja nyumbani na mshiriki mmoja atakaeperform wimbo wangu kwenye kipengele cha Vipaji kwenye mashindano ya urembo ya (Miss Indian Ocean)na inabidi tumvalishe kama mimi nikamwambia sawa!walipofika nyumbani
“Kwangu nilimwangalia wema juu mpaka chini na alivyo mrefu,nikamwambia Mange huyu anashinda Miss Tanzania,nakumbuka alikuwa mwembamba,mrembo na mwenye aibu and I was like Wow!!!!Anyway kiufupi Nakupenda mpaka leo Wema,Maisha ni Kama milima!wewe bado ni mdogo sana na una nafasi ya kuwa utakacho!”
“Pamoja na yanayoendelea sasa bado moyo wangu una imani na wewe kuwa utasimama tena zaidi ya juzi jana na leo na Utakua.Never give up!Dunia inaweza kukubadilikia kutoka kuwa kipenzi cha watu na kuwa Public enemy number one!Its normal!!!Its ok!ila kumbuka Familia yako ndio kila kitu!Please usihuzunike ukajiona wewe ndo mkosaji dunia nzima”
“Maana kila binadamu ana majanga yake ni Mungu tu ndio mkamilifu ingawa sio sababu ya kutufanya kurudia makosa over and over again!Nakupenda na nina imani na wewe!Nakutakia kila la kheri katika maisha yako na natamani kumuona Wema Mpya.Lots of 💖@wemasepetu”
Amber Rutty anaweza kufungwa maisha au miaka 30 jela