Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson anazidi kuingiza mkwanja mrefu wa pesa ingawa hayuko tena duniani, hiyo ni baada ya kuongoza katika list ya watu maarufu waliofariki dunia.
Katika jarida la Forbes limemtaja Marehemu Michael Jackson katika list ya ‘The Highest Paid Dead Celebrities 2018’ na kutaja kuwa mfalme huyo ameingiza kiasi cha zaidi ya Tsh Bilioni 917 tokea October 2017 mpaka October 2018.
Kiasi hicho cha fedha kinatajwa ni kutokana na asilimia 50 ya mauzo ya kazi za MJ kutoka EMI Music Publishing na kupelekwa kwenye kampuni ya muziki ya Sony/ATV pamoja na pesa kutoka kwenye Catalogue yake ya Mijac Music.
Project ya kipindi maalum cha televisheni cha ‘Michael Jackson Halloween’ kinatajwa pia kutoa malipo, kipindi hicho kilirejea kwenye kituo cha CBS cha Marekani October 20,2018 ikiwa kimefanyika miaka miwili mfululizo.
Hii ndio full list ya mastaa waliokufa lakini bado majina yao yanaingiza pesa nyingi kutokana na vitu walivyofanya enzi za uhai wao.
1. Michael Jackson ($400 million)
2. Elvis Presley ($40 million)
3. Arnold Palmer ($35 million)
4. Charles Schulz ($34 million)
5. Bob Marley ($23 million)
6. Dr. Seuss ($16 million)
7. Hugh Hefner ($15 million)
8. Marilyn Monroe ($14 million)
9. Prince ($13 million)
10. John Lennon ($12 million)
Askofu Gwajima na Kibonde walivyojichanganya kwa Masanja “Hilo ni pepo”