Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mpiga picha William Wilson amemshtaki Justin Bieber kutokana na tukio lililotokea mwaka 2017 baada ya Bieber kumgonga na gari wakati akitoka kanisani mjini Los Angeles.
William Wilson amedai mbele ya mahakama kuwa ni uzembe uliopelekea ajali ile na kusema alikuwa amesimama upande wa waenda kwa miguu na ndipo Justin Bieber alipolipeleka gari lake moja kwa moja na kumgonga.
Justin Bieber alijitetea na kueleza kuwa waandishi walishuhudia tukio hilo na hakufanya makusudi bali ajali hiyo ilitokea kutokana na matatizo ya kiafya.
Inadaiwa kuwa Justin Bieber alionyesha ushirikiano wa gari la wagonjwa kufika na kumchukua William, kwa upande wa taarifa za polisi wa Beverly Hills zilisema kuwa Justin Bieber alishirikiana nao vyema hivyo hakufunguliwa shtaka lolote.
AUDIO: ULIPITWA NA MHITIMU ALIEDUKUA MTANDAO WA WIZARA NA KUJILIPA MISHAHARA MIEZI 10? SIKILIZA HAPA KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI