Unaambiwa kuwa bifu lililopo kati rapper Nick Minaj pamoja na Miley Cyrus bado linaendelea hii ni baada ya kudaiwa kuwa Miley alimchana Nicki kwenye ngoma yake mpya ya ‘Cattiude’ nakusema kuwa anampenda Nicki lakini anasikiliza nyimbo za Cardi B.
Kupitia mahojiano aliyoyafanya Nicki Minaj kwenye episode mpya ya kipindi chake cha Queen Radio amefunguka na kudai kuwa aliwahi kumkuta Miley Cyrus akifanya mapenzi ndani ya studio na mtayarishaji wa muziki Mike Will Made-It na kusisitiza kuwa Miley amekua akifanya hivyo mara kadhaa ili atoke kimuziki.
“Nilishawahi kumuona Miley Cyrus akifanya mapenzi studio na Mike Will, kwahiyo unafanya mapenzi na kila mtu ili tu uonekane kwenye steji, kuku waliopotea hawawezi kumuongelea Malkia vibayana alinikosea heshima kwenye gazeti bila sababu” >>>alisema Nicki Minaj
Inaelezwa kuwa bifu kati ya Nicki Minaj na Miley Cyrus lilianza kuonekana mwaka 2015 baada ya Miley kumkosoa Nicki kupitia gazeti la New York Times baada ya kuwa na malalamiko juu ya tuzo za VMAs kumnyima tuzo ya video bora ya mwaka kwenye ngoma yake ya Anaconda.
https://youtu.be/TrwwzFtzbXw
VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MISS KINONDONI 2019 “HATUANGALII UZURI, TUNAANGALIA HESHIMA”? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.