Jumla ya Wafungwa 252 Mkoani Kigoma wameachiliwa huru kupitia msamaha wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli huku wakiahidi kuwa wazalendo wa Nchi.
Wakizungumza mara baada ya kuachiwa huru baadhi yao wamesema maisha ya jela yamekuwa sehemu ya Chuo kwa kutoa elimu na kwamba watakuwa sehemu ya kutoa elimu kwa watu wengine ili kuepukana uhalifu na kufanya kazi za maendeleo.