Michezo

Simba SC yamrejesha Seleman Matola

on

Simba SC leo imetangaza rasmi kuwa kocha Seleman Matola amerejea katika timu hiyo na kujiunga nao kama kocha msaidizi akitokea club ya Polisi Tanzania aliyokuwa anaitumikia tena kama kocha msaidizi pia.

Matola anajiunga na Simba SC kwa mara nyingine baada ya miaka kadhaa kupita ambapo alikuwa kocha msaidizi Simba SC chini ya kocha wa zamani wa Simba SC Dylan Kerr, Simba SC imeahidi kuwa itatangaza kocha mkuu wa timu hiyo wiki ijayo baada ya kuachana na Patrick Aussems.

“Najisikia furaha kwa sababu nimekuwa mchezaji wa zamani wa Simba SC lakini nilikuwa kocha msaidizi wa Polisi Tanzania sasa naweza kurudi nyumbani kubwa ni kuja kushirikiana na benchi la ufundi kuhakikisha tunaisogeza Simba SC kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine”>>>Matola

VIDEO: PAMBANO LA ROUND 10: MWAKINYO VS TINAMPAY

 

Soma na hizi

Tupia Comments