Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mbeya mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” amekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Mbeya muda mfipi baada ya kuchukua fomu za kugombea ubunge katika ofisi za msimamizi wa uchguzi.
Sugu amekamatwa baada ya majibishano baina yake na afisa wa polisi aliyefika na kumueleza sababu za kumkamata wakati akijiandaa kufanya mahojiano na waandishi wa habari kuwa ni kufanya maandamano bila kibali.